VIPI KAMA WALIVYO NDIVYO TULIVYO?
Wakati mwingine tunadhani zamani ndiyo mengi ya hovyo yalifanyika
Wakati mwingine tunadhani waliokuwepo ndiyo waliotufikisha tulipo
Wakati mwingine tunawalaumu wengine ili kuwafanya wengine watupende.
Lakini baada ya kuwepo tulipo kwa muda tunagundua mengi ya hovyo bado yanafanyika
Ndipo tunajua kuwa kumbe tulipojikuta tulistahili kuwepo kwa jinsi tulivyo
Ndipo tunajua kumbe tulipo hatukufikishwa na mtu mwingine yeyote, tulijifikisha mwenyewe
Na hapo ndipo tukiendelea kuwalaumu tulionao hapo, watu wenye akili wanatushangaa
Maana wenye akili wanakuwa wamejua walivyokuwa ndivyo tulivyo
Hatuna tofauti!
© Mathias Masaka

Comments
Post a Comment