Posts

Showing posts from April, 2020

KIFO WAKATI UPO HAI

Image
“Unakufa ukiwa na miaka 20 unazikwa ukiwa na miaka 60’’ Nilikuwa nasoma kitabu kimoja nikakutana na sentensi hii, ikanifikirisha kidogo. Nikataka kujua mwandishi wa kitabu hicho alimaanisha nini kusema watu wengi hasa Afrika, wanakufa wakiwa na miaka 20 lakini wanazikwa wakiwa na miaka 60? Katika kujifunza zaidi nikagundua tabia 08 zinazoweza kuonyesha mtu aliyekufa lakini angali na uhai ndani yake. 1. Kuamka na kulala bila ratiba maalumu. Hii ni tabia inayowakumba vijana wengi wasomi na wasio wasomi. Utamkuta mtu na familia yake kabisa lakini anaamka asubuhi anajiuliza au anasemezana na mwenzake leo sijui niende wapi, sijui nifanye nini! Utasikia oyaa! Una mchongo wowote huko? Akiambiwa hakuna anarudi kulala asubirie chai au ugali wa mchana. 2. Kutoishi katika uhalisia. Hii ni tabia waliyo nayo vijana wa kitanzania. Kupenda kumiliki vitu vya kujionesha visivyoendana na uhalisia wa maisha yao. Mathalani mtu yuko radhi auze mtaji wake wote wa kuku ili amiliki iPhone....

UGONJWA WA CHUKI

Image
@yurisdutch Yurisdutch@gmail.com Je umewahi kuchukiwa na watu pasipo sababu zozote?Umewahi kusikia  juu ya watu wenye chuki BINAFSI? Je umewahi kujiuliza ni sababu zipi  zinasababisha watu wakuchukie?🤔🤔🤔🤔 Kuna wakati katika Maisha kuchukiwa ni kawaida kabisa hasa wakati utakapoanza kuchanua na kung'aa katika kile unachokifanya. Lakini hebu tujiulize kwa umakini kabisa hivi kwann watu wanatuchukia??Wivu ni moja ya jibu kati ya majibu mengi utakayoyafikiria  juu ya sababu ya MTU kuchukiwa.Endeleeea Pindi unapoanza kung'ara na kuwa bora katika nafasi yako,wapo wengi ambao walijaribu Kufanya kama unachokifanya wakashindwa,wapo wengi ambao hata robo ya nafasi yako hawakufika  walipojaribu Kufanya jambo unalolifanya kwa hiyo usiogope kuchukiwa kabisa.Wengi watakuchukia wakidhani haustahili kuwa pale ulipo,na wanadhani WAo ndio wanastahili Zaidi. Watu wengi huona ni heri afanikiwe MTU wasiye mfahamu kuliko ufanikiwe wewe wanaokufahamu kwa  hiyo ni kaw...

USIKATE TAMAA CHANGAMOTO NI MTAJI

Image
Kaaribu tena katika wasaa mzuri wa kutiana hamasa juu ya maendeleo na mafanikio katika safari yetu ya maisha hapa duniani. Changamoto zimekuwa kikwazo kwa watu wengi kushindwa kufikia mafanikio yao ambayo wamejipangia kupitia mikakati au mipango yao waliopanga kuifikia kwa muda Fulani. Rafiki naomba nikutie moyo kuwa changamoto ni mtaji wa mafanikio katika safari yako ya mafanikio, usikate tamaa kwani utakuwa unajirudisha nyuma ili uanze tena chini. Wakati unaanza utakumbana na changamoto zingine ambazo zinaweza kukufanya hata uone kuwa ni uchawi badala ya kukazana kuzitatua hizo changamoto. Habari njema ni hii, kuna msemo mmoja unasema ‘Mzigo huwa mzito unapokaribia nyumbani’, pia ‘Giza huwa nene kunapokaribia kucha’ hivyo kuna nuru katika changamoto, cha msingi ni kutafuta njia ya kuzishughulikia hizo changamoto kwani ukizitatua ni njia moja kwa moja ya kuelekea kilele cha mafanikio! Hebu angalia pia Mwandishi na Mhamasishaji mahiri barani Afika kutoka Tanzania, Eric Shigo...

Quote pic 002

Image
Welcome Utre News loves You 

NIDHAMU BINAFSI-001

Image
NIDHAMU BINAFSI SEHEMU YA KWANZA instagram @ Yurisdutch Yurisdutch@gmail.com Kuna wakati unapoanza Kufanya jambo unalianza kwa Nguvu zote na kwa Hamasa kubwa sana,kuna wakati MTU anapoanza Kufanya jambo analifanya kwa juhudi sana na kujituma lakini kadiri muda unavyokwenda ndivyo MTU huyo anavyopoteza passion/Hamasa ya kuendelea kulifanya kwa kiwango kile kile alichoanza nacho. Mtu mmoja aliwahi kusema " What distinguishes the truly successful person from the average person is the ability to understand why you are feeling demotivated " Kinachomtofautisha MTU aliye fanikiwa na MTU wa kawaida katika mafanikio  ni ule uwezo wa kuelewa kwa nini Hamasa aliyokuwa nayo hapo mwanzo imepungua.watu wenye kuhitaji kufanikiwa siku zote huitikia katika sababu ya kupungua  kwa Hamasa na kuifanyia kazi.Watu wengi tunashindwa kujiuliza ni jambo gani liliondoa Hamasa yetu katika kile tunachokifanya matokeo yake tunarudi nyuma badala ya kupiga HATUA. Ni vigumu kupata Amani kama h...

Quote Pic 001

Image

MAAMUZI MAGUMU

Image
Habari ,Leo hebu tulidadavue hili kidogo. Unajua wakati unamfundisha mtu kitu yawezekana kabisa uliona kama anakuelewa kumbe hujui kuwa hakuelewa,, sasa Lengo langu halipo kwenye kufundishana, nimelenga kwenye kusaidia Ni vigumu kujua shida ya mtu iwapo upo mbali naye utatudanganya bure kumbe mnafki. Ukitaka kuelewa kwamba kweli watu wengi unavyowaona sivyo walivyo watakuonyesha sura nzuri kumbe wanashida nyingi sana. Hebu jaribu leo kuishi na mshikaji wako huyo ndo utajua kuna shida hatari UNAWEZA KUTA --huwa hatandiki --miguu inanuka --mbinafsi --hafui taulo  --mvivu --hapendi kazi  --ana dharau sana kitaa hapo  --mpenda sana sifa N. K sasa hayo yote na mengine mengi huwezi yajua kama huwa mnakutanakutana tu maeneo flani,hasa kwenye mahusiano unavimba kitaa kwamba una bonge la mpenzi kumbe ana tabia chafu ila umbali mlio nao hauwezi kujua. Ngoja nikushauri kitu, usipende kuamini kitu kwa haraka sana, kuwa mtafiti ,elewa ukweli. ANGALIA MTU WANGU WASI...

INSTAGRAM class 01

Image
najua wengi mnafahamu kuhusu tags au mmesikia au mnazitumia. Naomba tuendelee na hili darasa mambo ya kawaida kama haya kisha tutaleta zile nondo kubwa kubwa. Sasa Leo tuangalie matumizi sahihi ya tags Hizi # tags zina umuhimu sana kuongeza viewers wa post yako, mfano mm 75% ya wanaoview nawapata kwenye tags Jaribu kufuatilia tags zinazotrend kwa sasa na ww uzitumie hizo hizo Angalia kwenye post za watu wanapendelea tags gani Kisha kama zinakufaa na wewe zitumie 💪🙏🙏.