MAAMUZI MAGUMU
Habari ,Leo hebu tulidadavue hili kidogo.
Unajua wakati unamfundisha mtu kitu yawezekana kabisa uliona kama anakuelewa kumbe hujui kuwa hakuelewa,, sasa Lengo langu halipo kwenye kufundishana, nimelenga kwenye kusaidia
Ni vigumu kujua shida ya mtu iwapo upo mbali naye utatudanganya bure kumbe mnafki.
Ukitaka kuelewa kwamba kweli watu wengi unavyowaona sivyo walivyo watakuonyesha sura nzuri kumbe wanashida nyingi sana.
Hebu jaribu leo kuishi na mshikaji wako huyo ndo utajua kuna shida hatari
UNAWEZA KUTA
--huwa hatandiki
--miguu inanuka
--mbinafsi
--hafui taulo
--mvivu
--hapendi kazi
--ana dharau sana kitaa hapo
--mpenda sana sifa
N. K
sasa hayo yote na mengine mengi huwezi yajua kama huwa mnakutanakutana tu maeneo flani,hasa kwenye mahusiano unavimba kitaa kwamba una bonge la mpenzi kumbe ana tabia chafu ila umbali mlio nao hauwezi kujua.
Ngoja nikushauri kitu, usipende kuamini kitu kwa haraka sana, kuwa mtafiti ,elewa ukweli.
ANGALIA MTU WANGU WASIKUPOTEZE 💪💪.

Comments
Post a Comment