UGONJWA WA CHUKI


@yurisdutch
Yurisdutch@gmail.com



Je umewahi kuchukiwa na watu pasipo sababu zozote?Umewahi kusikia  juu ya watu wenye chuki BINAFSI? Je umewahi kujiuliza ni sababu zipi  zinasababisha watu wakuchukie?🤔🤔🤔🤔

Kuna wakati katika Maisha kuchukiwa ni kawaida kabisa hasa wakati utakapoanza kuchanua na kung'aa katika kile unachokifanya.

Lakini hebu tujiulize kwa umakini kabisa hivi kwann watu wanatuchukia??Wivu ni moja ya jibu kati ya majibu mengi utakayoyafikiria  juu ya sababu ya MTU kuchukiwa.Endeleeea

Pindi unapoanza kung'ara na kuwa bora katika nafasi yako,wapo wengi ambao walijaribu Kufanya kama unachokifanya wakashindwa,wapo wengi ambao hata robo ya nafasi yako hawakufika  walipojaribu Kufanya jambo unalolifanya kwa hiyo usiogope kuchukiwa kabisa.Wengi watakuchukia wakidhani haustahili kuwa pale ulipo,na wanadhani WAo ndio wanastahili Zaidi. Watu wengi huona ni heri afanikiwe MTU wasiye mfahamu kuliko ufanikiwe wewe wanaokufahamu kwa  hiyo ni kawaida sana kuchukiwa.Ukiwa na wivu wa kijinga katika Maisha yako basi hutakuwa  na sehemu katika mafanikio,Penda kuona watu wengine wanafanikiwa ,kama una nafasi watie moyo wenzako,acha ubinafsi   kabisa na kamwe usiupe moyo wako nafasi ya kutunza wivu usiofaa maana wivu ukizidi  unazaaa chuki zenye maumivu ndani yake.

HATUA zako za kimaendeleo zimekuwa ni kama msumari wa nchi moja na nusu unaochoma katika mioyo yao kiasi kwamba wanaumia wanapoona tabasamu lako.Jinsi unavyozidi kupiga HATUA kusonga mbele wapo wengi watakaoona wivu na wapo pia wengi watakaoingiza  wivu ndani ya mioyo  yao na kuindekeza hatimaye watakuchukia kabisa.

Kila utakachokuwa unakifanya kwao  itakuwa ni kibaya,hata kama utafanya vizuri vipi bado kazi yako bora haiwezi  kubadilisha chuki zao.Usipoteze muda wako kuhangaika ili kila MTU akupende,Wale unaowatarajia na kudhani kuwa wanakupenda wengi huhifadhi chuki mioyoni  mwao  na kutoa tabasamu LA unafiki mbele yako.

Terry mark  aliwahi kusema  "No matter how good you are people are going to hate you ,people are going to be against you but never let them to be the limit of your success"
Akimaanisha "hata uwe mwema kiasi gani,watu watakuchukia tu,watu watakupinga tu katika kile unachokifanya lakini kamwe usiruhusu chuki zao zikawa kikwazo katika mafanikio yako"

Ni kweli huwezi kuzuia watu wasikuchukie lakini unaweza kubadili mtazamo wa chuki zao kama changamoto yenye fursa ndani yake.Siku zote unatakiwa ujue watu wenye chuki hawana rangi  kwa hiyo yoyote yule anaweza akakuchukia na wakati wowote ule.Jifunze namna ya kudili na kuwashughulikia watu wenye chuki katika Maisha yako.

Chuki haiui wala kukuondoa katika mstari endapi utaweka mtazamo chanya katika hiyo.

Wapo wengi unaowapenda na kuwaamini sana tena una wathamini mno lakini kuna muda haohao ndio watakuwa watu wa kwanza kukusema vibaya na kukuchafua sifa kabisa.Lazima utambue nafasi ya chuki za watu katika kuharibu mafanikio yako ikiwa utaruhusu ikuumize moyo wako.

Binadamu Mwenye chuki juu ya mafanikio ya wengine sio mbaya lakini ile sifa iliyopo  ndani yake ndio mbaya.Jifunze namna ya kushughulika na watu wenye chuki katika mafanikio yako na katika Maisha kiujumla.

Yurisdutch@gmail.com
Choices and decisions 2020


Comments

Popular posts from this blog

Life full of success just like the chinese bamboo tree

TENGENEZA POST TOFAUTI

COMMENTS NI PESA