MAMBO MATATU YANAYOUA HAMASA YAKO

@yurisdutch
yurisdutch@gmail.com


Kusonga mbele katika Maisha ni jambo ambalo kila mmoja analihitaji  ili kuweza kutimiza malengo bainishi aliyojiwekea.Katika kusonga mbele unahitaji kuwa na ari yenye kukutia  moyo na Nguvu ili kila siku unapoamka asubuhi uwe na Nguvu Mpya ya kukufanya uendelee Kufanya kile ulichokuwa ukikifanya kwa kasi na ubora Zaidi.

Wengi tunapokuwa katika mapambano mwonekano wa hali tunayoiona unaturudisha nyuma kwa kiasi Fulani kiasi kwamba ile hamasa tuliyokuwa nayo hapo mwanzo inaanza kupungua  siku baada ya siku.

Ulianza kwa kasi sana Biashara yako na ikawa inachanua vizuri lakini tangu changamoto zianze kujitokeza katika Biashara yako ile Hamasa uliyokuwa nayo imeshuka sana,unajikuta  una kosa Nguvu za kuendelea Kufanya Biashara katika hali ile ile au Zaidi ya ile uliyoanza nayo hapo mwanzo.

Sasa siku ya Leo tutaangalia vitu/mambo matatu hatari ambayo ukiyakosa katika Maisha yako hasa katika kile unachokifanya yanaweza kuwa chanzo cha wewe kurudi nyuma kutokana na kukosa Hamasa ya kuendelea Kufanya unachokifanya kwa kasi na ubora uleule uluoanza nao au Zaidi yake.Haya mambo matatu ndio yanayoua Hamasa yako(motivation killers).

(1) KUKOSA KUJIAMINI
     Moja ya kosa kubwa unaloweza kulifanya  katika Maisha yako ni kukosa kujiamini. Usipojiamini wewe usitegemee kushinda katika chochote kile hata maandiko yanathibitisha hili.Lazima uamini juu  ya uwezo wako,lazima ukubali juu ya vile ulivyo,lazima uishi  MAISHA yako.Usikubali kupoteza focus yako kutokana na kuyumbishwa na kelele za watu.Wengi hawatakuamini ila  ukijiamini hata kile kinachotisha sana utakiona ni kitu cha kawaida.

Ni kweli hauwezi kuendelea Kufanya jambo ambalo huliamini,na kama ukiendelea kulifanya  jambO hilo basi jua unajiandaa kufeli.Ukikosa kujiamini basi zile kelele zinazokukatisha tamaa zinakuwa kitovu cha Hamasa yako kushuka.Jifunze kutengeneza kujiamini sana ili uinue Hamasa YAKO katika kile unachokifanya.

(2) KUKOSA UMAKINI

Kinachomtofautisha MTU aliye fanikiwa na asiyefanikiwa sio tu namna wanavyofikiri au kutenda Bali hata UMAKINI wanaovipa vitu vyenye kuwainua.Ukiwa MAKINI kamwe hauwezi  kupotea  kwani MTU MAKINI huwa na tahadhali  kubwa.Saizi kuna wimbo LA watu wengi kutaka kuwa maarufu,kwa hiyo watu wengi wanatoa mawazo ya namna mbali mbali na yenye kujenga lakini kama hautakuwa MAKINI mawazo hayo hayo mazuri yanaweza kukuondoa kwenye mstari kwa kukupotezea umakini katika kile unachokitafuta.

Kuanzia Leo anza kufikia maanani juhudi zako na maono yako,mbinu zako na mawazo yako yaimarishe na kuyawekea msingi imara wa maarifa ili usitingishwe na mawazo mapya.Ukiwa MAKINI huwezi kupoteza Hamasa yako kwa sababu ya mawazo ya watu wengine.Pigania kuwa na Hamasa katika kuboresha Maeneo uliyo  bora Zaidi.

(3) KUKOSA MWELEKEO

Kama unajua ni kitu gani unakihitaji katika Maisha na unaamini  unaweza ukakitafuta na kukipata lakini ukawa hujui namna ya kuanza basi kuna mawili ,Aidha kupoteza Hamasa yako  au kuacha Kufanya kile unachokitaka na kuanza Kufanya kitu kingine.

Ni rahisi sana kukosa mwelekeo  katika Maisha kwa kutaka Kufanya kila kitu kinachokuja mbele yako na matokeo yake mwisho ni kabisa unakuja gundua umepoteza muda wako kwa Kufanya mambo yasiyo ya msingi na unakuwa umebaki nyuma sana.Hamasa yako inashuka na unajikuta  ni MTU Mwenye majuto.

Chagua mambo machache ya Kufanya katika wakati Fulani,Kama umepanga malengo mengi ya kuyatimiza ni vema ukaanza na machache uliyoyawekea kipaumbele."LIMIT YOURSELF TO FEWER GOALS AND YOU'LL ACHIEVE MORE"
🙏🙏🙏🙏🙏🙏

Kuna darasa linaendelea kila siku kupitia choices and decisions group
Telegram

Usisite kuacha uzoefu wako katika mambo haya matatu nami napenda kujifunza kutoka kwako.

@yurisdutch
Yurisdutch@gmail.com
Choices and decisions 2020


DOWNLOAD APP YETU HAPA

Comments

Popular posts from this blog

Life full of success just like the chinese bamboo tree

TENGENEZA POST TOFAUTI

COMMENTS NI PESA