TUKUMBUKE ZAMANI
@yurisdutch
Yurisdutch@gmail.com
Dr Sigmund Freud katika nadharia yake ya psychoanalysis anasema"Things that have happened to people during childhood make them behave in a particular manner in the present".
Vitu vilivyowahi kuwatokea watu katika kipindi chao cha utoto ndivyo vinavyowafanya wengi waonekane kama wanavyoonekana sasa.Maisha uliyoishi hapo zamani yana mchango Fulani katika Maisha unayoishi sasa, nidhamu uliyokuwa nayo zamani imechangia pakubwa mpaka wewe ukawa hapo ulipo,Marafiki uliokuwa ukicheza nao zamani au ulioweza Kufanya nao mambo mengi kwa pamoja wamechangia kwa kiasi Fulani mpaka wewe ukawa hapo ulipo,Tabia ulizoziishi pale zamani zimechangia kwa kiasi Fulani mpaka wewe kufika hapo ulipo.
Ni ukweli usiofichika kwamba MTU anayesahau mambo yaliyopita huenda akayarudia kuyatenda yaleyale aliyoyafanya zamani,kwahiyo naona kuna umuhimu wa kutunza mafunzo uliyoyapata kutokana na mambo uliyoyafanya hapo zamani ili ujilinde usifanye makosa Mengine.Kuna umuhimu wa kujifunza kutokana na marafiki uliokuwa nao hapo zamani,Fanya tathmini ya Maisha mliyoishi mkiwa pamoja,angalia challenges mlizokutana nazo,jaribu kuzitatua zilizo ndani ya uwezo ambazo ni za tangu mlipokuwa karibu,angalia ubora mliokuwa nao pindi mlipokuwa pamoja,Angalia mambo yaliyokuwa yanakukwamisha katika kipindi cha zamani,JE mpaka sasa bado yapo,fanya tathmini.
Tafiti zinaonyesha mambo madogo na yanayodharaulika na wengi ndio yanayowaangusha wengi.Wengi huwa tunadharau vitu vidogo vidogo na kuacha kuvipa muda wa kuvitafakari tunajikuta tuna kosa msingi imara wa Yale mambo makubwa tunayo yahitaji.
Ni kweli huwezi kubadili Yale mambo yaliyotokea zamani lakini unaweza ukabadili mtazamo juu ya mambo yenyewe.Makosa yaliyofanyika katika kipindi kilichopita yasikutishe wala kukukatisha tamaa,badili mtazamo juu ya mambo hayo,jenga mtazamo chanya ,yaone mambo hayo kama fursa ya kujifunza iliyojileta kwa mfumo wa changamoto.
Mambo uliyoyafanya zamani ni kweli yamechangia wewe Kuwa hapo ulipo lakini unaweza ukaanza hapo ulipo kutengeneza matokeo yatakayosomeka kitofauti hapo baadae.
@yuris Dutch
Yurisdutch@gmail.com
Choices and decisions 2020
Very good 👍
ReplyDelete