WEWE NI NANI?-sehemu ya pili


SEHEMU YA PILI
@yurisdutch
Yurisdutch@gmail.com

Kijana akamuuliza socrate "nini siri ya mafanikio"?
Socrate  akamjibu kwa kumuuliza "Ni kweli unataka kujua nini siri ya mafanikio"? Kijana akamjibu Ndio nahitaji  kujua.

Socrates akamwambia kesho alfajiri na mapema tukutane kando ya Bahari.Kijana akasema  sawa.

Ilipofika alfariji kiza kikiwa bado  kipo,kijana taratibu akaanza kusogea eneo alilokubaliana kukutana na mwalimu wake socrate.Akiwa kwa mbali  kidogo alimuona MTU amesimama kando ya bahari  bila shaka na alikuwa ni socrate.

Kijana alipofika mahali alipokuwa Socrates ,Socrates akamwambia tangulia ndani ya maji, kijana akatangulia ndani ya maji akiwa mbele Socrates akiwa nyuma yake,Jinsi walivyozidi kwenda mbele ndivyo kina kilivyozidi kuongezeka na ndivyo walivyozidi kuzama katika maji.Maji yalifika Maeneo ya shingoni mwa kijana ,Socrates akasema  stop.Kijana akasimama asijue mwalimu wake anataka kumwambia nini.

Gafla Socrates akamzamisha kijana katika maji kwa Nguvu.Kijana akiwa anahangaika kuchomoka katika maji lakini asiweze,Socrates alidumu kumzamisha kwa muda mchache ,kijana akiwa ameishiwa oksijen kabisa ndipo Socrates akamchomoa katika maji.

Alipumua kwa Nguvu sana huku akilalamika kwa nn alizamishwa ndani ya maji.Ndipo Socrates akamuuliza yule kijana Ni kitu gani cha muhimu ulichokuwa unakihitaji zaidi pindi ulipokuwa  ndani ya maji? ,kijana akajibu Ni oksijeni

Socrates akamwambia Basi hiyo ndiyo  siri ya mafanikio
Kama unahitaji mafanikio basi unahitajika kuyatafuta kwa hamu kubwa kama hamu ya kupata oksijen  uliyokuwa nayo pindi ukiwa ndani ya maji.

Kama unahitaji kujua wewe ni nani basi hauna budi kujifuatilia kwa umakini ili ujue wewe ni nani hauna budi kujifunza Zaidi ili kujua wewe ni nani.Hamu kubwa ya kujua wewe haitaisha bila kujifahamu Zaidi.Endelea

wewe ni nani? Ni swali LA muhimu sana na gumu  kulijibu na kama ikitokea MTU akashindwa kulijibu swali hili basi ujue atakuwa  MTU mwingine tofauti na MTU yule aliyepaswa kuwa,utakuwa ukitimiza majukumu ya watu wengine,utakuwa ukitimiza kusudi LA watu wengine,utakuwa MTU mwingine katika sehemu nyingine tofauti na MTU yule ambaye ungekuwa kama ungegundua wewe ni nani.

Siku zote usiishi ili kukamilisha safari ya maisha uliyoianza siku ukitungwa mimba Bali ishi kwa sababu una kusudi LA Kufanya hapa duniani.Kila mmoja alizaliwa kwa sababu kuna Zawadi ambayo ulimwengu unaihitaji  kutoka kwake na ni yeye pekee aliyepewa Zawadi hiyo kwa sababu kila mmoja ni wa pekee (unique) .

Ulimwengu unahitaji lile  kusudi LA pekee uliloumbwa kwalo.Kama hautajua kusudi LA wewe kuwepo duniani ni lipi basi itakuwa ngumu kujua wewe ni nani.

Ulimwengu utapoteza kitu cha thamani sana kama ukifa ikiwa hukufanikiwa kujua wewe ni nani.Zawadi yako uliyopewa na Mungu itazikwa katika makaburi pasipo kutumika katika ulimwengu huu.

Hebu fikiria ivi dunia ingekuwa imepoteza kitu cha thamani kiasi gani kama Thomas Edison asingegundua taa ya umeme?Ivi ingetokea kitu gani  kama mgunduzi wa Simu angeshindwa kutambua kusudi LA yeye kuwepo duniani? Ivi ni kitu gani kingetokea kama Steve jobs asingegundua Yale Macintosh? Je ingekuwaje kama Alexander Berry asingetambua kusudi LA yeye kuwepo duniani?.Una kitu kikubwa sana ndani yako ambacho ulimwengu unakisubiri kwani hiyo ni Zawadi yake kutoka kwa Mungu aliye juu nayo ndio kusudi LA kukutambulisha wewe ni nani.

Dunia itapoteza kitu cha muhimu sana kama hautambua kuwa wewe ni nani kama utashindwa kujibu swali hili dunia itakosa Zawadi Mungu aliyoipatia kupitia wewe.Dunia itapoteza utajiri mkubwa nao utazikwa pamoja na Vito vingi Vya thamani vilivyozikwa katika makaburi.

Je unataka kuishi hapa duniani kama MTU aliyekuja  kutembea? Au kama MTU Mwenye kusudi LA thamani alilopewa na Mungu?

Endelea kufuatilia mfululizo wa  masomo haya utapata Mwanga wa kujua wewe ni nani?

Pitia somo lenye kichwa kinachosema  SEHEMU mbili za UBONGO zinazoathiri maisha yako mwandishi ni Mimi Mwenyewe .

Karibu katika SEHEMU inayofuata  na nikusihi usikubali kuacha kufuatilua kujua wewe ni nani.Tukutane katika somo lijalo.

ASANTE
@choices and decisions 2020
Yurisdutch@gmail.com
Same name in social media

Comments

Popular posts from this blog

Life full of success just like the chinese bamboo tree

TENGENEZA POST TOFAUTI

COMMENTS NI PESA