USIJIFUNZE BILA MPANGILIO
Kujifunza ni vyema, ila tujifunze kwa utaratibu
Hapa Naongelea vitu kama course za online au mtandaoni kokote pale
Tatizo la wengi kila upepo wa elimu tukisikia tu una mafanikio basi hapo hapo unaacha nyingine unaidakia nyingine
Mara Leo ujifunze forex, hapo hapo dropshipping, Mara graphics Mara YouTube, Mara sponsored ads ,mara online marketing
Ngoja nikwambie kwa chochote unachojifunza kwanza kabla haujaanza kujifunza, fuatilia vizuri kwanza ili uridhike kama Kweli unatka kujifunza
Mwisho wa siku utadanga Danga 😀
Alafu ujikute umepoteza muda na umepoteza vya thamani zaidi
Ukianza maliza,
Soon tutaanza kuPata Maarifa kidogo kuhusu digital skills Kama YouTube,sponsored ads, online marketing n.k
Mkumbushe na mwenzako apakue app ya Utre News
Comments
Post a Comment