KWA NINI UWE NA YOUTUBE CHANNEL??


Ni assume una uelewa kidogo  kuhusu Youtube channel, but hata kama hauna usihofu
Na hizi ni baadhi ya faida za kuwa na Youtube Channel

Unaweza Ingiza Kipato.
Moja ya jambo linalowashawishi wengi kuwa na Youtube Channel ni swala la kuingiza kipato ,lakini watu wengi haujafahamu hicho kipato kinaingiaje na kivipi.
Hapa kuna njia nyingi kwenye kuingiza kipato
Kuna njia ya ads kutoka adsence by admob intergration.
Njia nyingine ni sponsored ads ambazo ni direct ,yan wewe na mdhamini wako.
Mfano tunaona millardayo.com huwa anapromote vitu kutoka GSM na kadhalika.
Pia kuna njia nyingne nyingi kama affiliate links 
Sitoelezea sana kuhusu hapo ila kwenye post zijazo nitaelezea vizuri
Pia kuna swali kuhusu malipo ,huwa wanalipa kupitia bank MasterCard 

Mashabiki pande zote za Dunia
Moja ya kitu muhimu kutoka Youtube ni kwamba unaweza pata mashabiki wengi kutoka pande nyingi duniani ,hivyo unajiongezea wigo wako wa kujulikana hata kufikia watu wengi sana.
Ila jambo kubwa hapa usilofahamu ni kwamba kadri unavyotazamwa na watu nje ya Tanzania basi kuna uwezekano mkubwa pesa unayopata kuwa nyingi hata kama views ni chache.
Naona kuna swali jipya limeibuka "views ngap napata sh ngap??"  Hili swali watu Wengi wanalo kuchwani ila nikutoe uoga kidogo na ushamba, views lazima wawe wameangalia ads zako hivyo unaweza kuwa na video yenye views nyingi na usipate kitu ,kama tu hamna ads kwenye video.
Hili nalo nitalielezea vizuri post ijayo ,usihofu utaelewa tu.

Unaongeza wateja wa kazi au bidhaa zako
Hapa tuwe makini kwamba,moja ya kitu kitakachokulipa zAidi ukiwa na Youtube Channel ni kuuza bidhaa au kuonyesha kazi yako
Hebu chukulia mfano una Youtube Channel kuhusu michezo alafu unawaambia watu kuwa unafanya delivery ya jezi kali na viatu vya michezo,hii inakuongezea kipato zaidi.So hapa unaweza tangaza kitu chochote kile na ukapata faida kwani wateja wapo.

Contents zako haziwezi kufa
Waoh hii ni faida kubwa sana ukiwa na Youtube Channel,yani hatutegemei mtandao utakufa leo ama kesho,yan tangu 2005 uanzishwe hadi leo unaonekana kukua tu na sio kufa.
Hii ni tofauti sana na mitandao mingi mingine, yan saa yoyote wakati wowote inaweza kufa na kazi zako zikapotea ila sio mtandao wa YOUTUBE.

Unajitangaza mwenyewe
Hii ni Faida kubwa sana,hivi haujawahi sikia watu wanasema "wee sawa tu,kisa unajulikana,ila nitakuonyesha tu" au "wamempitisha tu,si anajulikana" 
 Hiyo ni mifano tu ,hapa uelewa kwamba ukijitangaza mwenyewe unauzika vizuri,ndio maana watu kama diamond kutokana na kazi nzuri na kujitangaza kwingi leo amekuwa ana gharama kubwa sana 
Hivyo Youtube itakusaidia kuonekana na kujulikana zaidi na kukuza jina lako.

Inaendesheka hata kwa simu
Hii ni sababu nyingne naweza sema !!
Unajua ukiwa na Youtube Channel unaweza kuiendesha hata ukiwa na simu mfano huwa tunatumia Youtube Studio iliyopo playstore kuendeshea YOUTUBE channel 
Kuna vitu vingi unaweza kufanya ukiwa na Youtube Studio app
Pia kuna baadhi ya app nzuri za kuedit video na picha kama Kinemaster na pixellab 
Hizo zote ni unatumia simu tu
Pia ukitaka kushare videos zako unatumia simu
Kwa sababu hii kuna urahisi kidogo kuendeshea YOUTUBE channel yako.

Mtandao wenye watu wengi
Uzuri ni kwamba sio wewe ndio utakuwa wa kwanza kutumia YOUTUBE ni mtandao wenye wafuasi wengi sana duniani
Hivyo ni wewe tu na akili yako ufanye nini,maana kama wafuasi tayari wapo wakutosha.

Unaongeza uwezo wa kubuni na kufikiri
Hii ni faida nyingne unaweza kuipata ukiwa na Youtube Channel,kwani uwezo wako wa kufikiri na kubuni utaongezeka zaidi.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba utatumia akili nyingi kutaka kufanya vitu vizuri zaidi ,hivyo wakati huo na wewe uwezo wako wa ubunifu na kufikiri unaongezeka zaidi

Miaka michache baadae lazima utahitaji
Kutokana na ukweli kwamba kama unataka kufanya biashara yenye wateja wengi,zunguka uzungukavyo,waza uwezavyo ,wazo kuwa na Youtube Channel litakuja tu ,ila labda ukose atakayekupa mwongozo ndipo wazo life 
Nimekutana na watu wengi wakiniuliza kuhusu Youtube Channel na wana kazi zao.
Maana swala la YOUTUBE channel sio lazima liwe kuhusu kazi yako hiyo
Mwingine anaweza anzishA kama sehem ya biashara nyingne.
Contacts 0766346065///0625645425

Asante sana,nakushukuru kutuchagua,tafadhali download Utre News app ,pia mwambie mwenzako kuhusu App hii usiwe mchoyo ,tunawapenda.


Comments

Popular posts from this blog

Life full of success just like the chinese bamboo tree

TENGENEZA POST TOFAUTI

COMMENTS NI PESA