USHAWAHI KUJIULIZA UTU NI NINI? 

Utu ni neno ambalo tunalitumia sana katika maisha yetu ya kila siku. Si ajabu wengine wanalitumia bila kujua maana halisi ya neno hilo. Ushawahi kujiuliza neno hilo limebeba maana gani? Wakati mwingine unaweza kusikia watu wakisema, "huyu jamaa hana utu kabisa hafai kuigwa" unadhani wanamaanisha nini?
 
Basi leo ungana nami tujifunze kitu.

Kwa kuangalia jinsi neno linavyotumika katika jamii yetu, tunaweza kusema Utu ni kusaidia na kujali wengine bila  kuangalia tofauti zilizopo katika maisha kama vile maumbile, elimu, kipato nk.. Au kusaidia wengine bila kutegemea kupata chochote kama faida ya msaada wako. Kutokujiona wewe ni bora na kudharau wengine kwa namna yoyote ile. Pengine kuna maana nyingi zaidi lakini kwa leo acha tujadili hizo.

Kuna watu hujiona bora kuliko wengine kwasababu ya elimu yao. Wengine hudiliki kusema, "yule jamaa si lolote si chochote hata darasa la saba hakufika atanishauri nini mimi na shahada yangu" cha msingi hapa si elimu yako kubwa, je unatumia vipi elimu yako kuishi na watu vizuri katika familia na jamii kwa ujumla, elimu yako inasidia vipi wengine? Au elimu yako haijakukomboa? Unachopaswa kuelewa ni kwamba kuna elimu ya darasani na elimu ya dunia au maisha. Pengine huyo unaemdharau na kumuona si lolote kisa elimu yake ndogo ana elimu ya maisha na anajua mambo mengi zaidi yako ni jambo la kumpa nafasi tu. Acha kujikweza na kudharau wengine, kama unataka kumsaidia mtu msaidie kwa moyo wako wote. Usiache kuwasaidia watu kisa tu wana elimu ndogo. Huko ni kukosa utu. 

Kuna watu hujiona bora kuliko wengine kwasababu tu wamekamilika kimaumbile. Mtu hujiona bora kisa tu ana mikono inayofanya kazi, miguu inayotembea, macho yanayoona, na masikio yanayosikia. Hii dunia ina mengi sana, na mwenye hii dunia Mungu kaumba watu na vitu vya aina tofauti. Kuna wenye masikio lakini hawawezi kusikia, kuna wenye macho lakini hawawezi kuona, kuna wenye midomo lakini hawawezi kuongea. Je, tuwadharau na kuwaona si kitu kwetu? Kama umeamua kusaidia watu saidia bila kuangalia mapungufu kwenye viungo vyao, eti huyu ni kipofu atanifaa nini mimi!? Anaweza asikufae leo ila akakufaa kesho au asikufae wewe bali kizazi chako. Saidia watu wote kwa usawa na huo ndio utu.

Tuseme ahsante kwa siku ya leo. Karibu katika uwanja wa maoni, tuambie umejifunza nini au unataka kumfundisha nini mwandishi na watu wengine kuhusu somo la leo?

Maoni yako ni muhimu sana. Karibu!

Comments

  1. Utu ni neno pana na linaweza lisiwe na tafsiri moja tu.
    Kimantiki utu ni ile hali ya kujali ubinadamu, kwenda kinyume na hapo ni kutokuwa na utu, waingereza wanaita against humanity.
    Tunapo zungumzia ubinadamu ni ile hali ya kuwa sisi binadamu tuna ufahamu mkubwa kuliko wanyama, kwamba hatuwezi kuishi kama wanyama tuna misingi yetu kama binadamu, kwa kuwafanyia wenzetu yale tunayopenda kufanyiwa na si yale usiopenda kufanyiwa.

    Mimi si mtaalamu wa lugha nashindwa namna mzuri ya kuliweka hili neno lieleweke uzuru
    Sasa kwa mfano FF anapo muita marehemu alikuwa mlevi au kichaa na ametoa kauli hiyo akijua si kweli wakati wenzake ndugu na na jamaa wanaomboleza kifo cha ndugu yao mpendwa, hapo ni kukosa utu, amekosa ile hali ya kawaida ya ki binadamu kutoa kejeli wakati wenzake wako katika wakati mgumu, na kumfanya marehemu ni kama hana thamani kwani alijitakia.

    Kwa issue ya mbunge, ukiangalia kwa manti mleta hoja anajua kabisa sheria zipo zinazotoa mwongozo kwenye jambo la ugonjwa kwa viongozi, lakini yeye ameweka kando kwamba kuna mtu kama yeye anapigania maisha yake apone na anapaswa kupewa sapoti kama binadamu yeyote, lakini kwake kwakuwa si wachama chake anaona anyang'anye ubunge kwa kuwa hafai ni mgonjwa na watafute mwingine

    Utu ni zaidi ya sheria inavyo weza kutafsiri, utu ni namna mtu anavyoweza kutendea wenzake kwa kadri ya matarajio ya jamii husika inavyotarajia binadamu wa kawaida kufanya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante sana kwa kuzidi kutujuza zaidi kuhusu utu. Huenda maoni yako yakawa faida kwa wote. Karibu wakati mwingine.

      Delete
  2. Replies
    1. Ahsante karibu wakati mwingine. Usisahau kukaribisha marafiki zako pia

      Delete
  3. Ahsante kwa somo zuri, nimelipenda mnoo...nimejifunza kusaidia watu bila kuangalia hadhi zao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante. Karibu wakati mwingine. Usisahau kuwaarika marafiki zako pia

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Life full of success just like the chinese bamboo tree

TENGENEZA POST TOFAUTI

COMMENTS NI PESA